Mashindano ya urembo nchini |
Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili
mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na
kanuni.Mashindano hayo
yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana
na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.Kwa mujibu wa
kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey
Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza
mashindano hayo.Alisema bwana
Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili,
lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali
kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao
umekuja kutokana na sababu maalumu,"Imedaiwa kuwa
mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao
mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo
kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa
waandaalizi kujipanga upya.Baadhi ya
maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa
kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia
vitongojini hadi kufikia fainali.Mngereza alisema
baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya
kuwa na sifa zilizohitajika
No comments:
Post a Comment