Rais Uhuru Kenyatta |
Kenyatta anasema
kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi
kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab. Amesisitiza kuwa
sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge
wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho
kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu
spika.Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu
kutoka kwa wabunge hao.
Vyombo vya
habari vimesema baadhi ya vipengee vya sheria hio ninabana uhuru wa vyombo vya
habari na hata kutishia kwenda mahakamani.Mswada huo kabla ya kutiwa saini na
kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo
vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na
katiba.
Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za
uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.Polisi pia ndio
watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au
kuonyeshwa katika vyombo vya habari.
Vyombo vya habaro vinasema haya yanakwenda kinyume na uhueu wa vyombo
vya habari.Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya
shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka
mitatu.
No comments:
Post a Comment