Umasikini na Ukeketeji watoto wa Kike |
Kwa muujibu wa desturi za serikali
za mitaa,sheria ya kutahiri wanawake,ina maanisha ni kipindi cha mpito kwa
binti kutoka kuwa msichana hadi mwanamke kamili,na hii inaashiria kwamba yuko
tayari kwa kuolewa.
Wasicha mia moja kumi na nane kati
yao wana umri wa miaka 10 hadi kumi na sita, wamehifadhiwa katika makazi salama
na vituo vinavyoendeshwa na kanisa la Anglikan huko Mugumu, wilayani
Serengeti.Rhobi Samwel ni mratibu wa mradi uitwao tunaweza ambao husghulika
zaidi na kuupinga ukatili wa kijinsia.kwa muujibu Rhobi anaeleza kwamba mapema
mwezi huu aliwaona mabinti hao wakiwa wamejikusanya kwenye vikundi,wengi wao
wakiwa katika hali mbaya na hivyo kuwapeleka katika mazi salama.
Wasicha walio wengi wametokea
wilayani Butiama,Tarime na Serengeti.miezi ya December na Januari ndio msimu wa
tohara kwa wasichana na wavulana kwa mkoa wa Mara.viongozi wa maeneo husika
wansema kwamba kupambana na kitu kinachoonekana kama ibada ya kitamaduni
utamaduni ni suala nyeti na endelevu .
Sijali Nyambuche ni afisa wa polisi
anayeshughulikia dawati la masuala ya jinsia na uangalizi wa wanawake na watoto
huko Mugumu,Serengeti.Yeye anasema pamoja na masuala yanayohusiana na hatari za
kiafya,jamii zimeendelea kushikilia msimamo wa kudumisha mila hiyo isiyo faa na
hivyo kudumaza juhudi za kumaliza tohara mkoani humo.Sophia Simba, waziri wa
maendeleo ya jinisa na watoto ana fafanua juu ya ukweli kuwa mara nyingi
wasichana hukutwa wakiwa tayari wameshafanyiwa tohara ;
Kwa muujibu wa sheria ya makosa
maalumu sheria ya mwaka 1998 ina kinza suala la tohara hutekelezwa kwa
wasichana walio chini ya umri wa miaka 18,lakini sheria hiyo haitoi ulinzi ama
tamko lolote mara baada ya wasichana hao wanapovuka kizingiti cha umri
huo.adhabu kwa kosa la tohara ni kifungo cha miaka mitano hadi kumi na mitano
.Ukatili huu umekuwa ukipungua tangu nchi ya Tanzania ilipopiga marufuku
vitendo hivyo mnamo mwaka 1996 na hii imechangiwa na kampeni za kuijengea uwezo
na kuielimisha jamii zilizokuwa zikiendeshwa na vikundi vya haki za binaadamu .
No comments:
Post a Comment