Mschana Hakika Abdalah. |
Bwana Mkaruka amefichua hili wakati
alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu katika mkutano uliolenga kuzungumzia
maswala muhimu ya elimu katika jimbo hilo.
Miongoni mwa maswala mengine, wadau
walizungumzia changamoto zinazowakumba wanaume katika elimu ya ngono chini ya
mradi wa TMEP.
Kulingana na Bwana Mkaruka ,idadi
hiyo inashirikisha wasichana walioshika mimba na kuwacha shule katika ya mwaka
2010 na 2014.
Amesema kuwa idadi hiyo
inashirikisha wasichana 59 kutoka shule za msingi na 749 kutoka shule za upili.
Nyumbani kwao Hakika Abdalah. |
Ameongezea kuwa wilaya ya Nkasi
ambayo ipo katika sehemu ya ziwa Tanganyika inaongoza na wasichana 477 ambao
walishika mimba na kuwacha shule.
Aliongezea kwamba miongoni mwa
wasichana 477,31 walikuwa wakisoma katika shule za msingi huku 446 wakiwa
katika shule za upili.
Kulingana na Mkaruka ,tatizo hilo
limekuwa likiongezeka kutokana utamaduni uliopitwa na wakati ambao unawaruhusu
wazazi kuwaoza wanao hata iwapo wapo shuleni.
''Ni wazi kwamba tunakabiliwa na
changamoto katika eneo hili,wazazi wengi bado wanaamini tamaduni ambazo tayari
zimepitwa na wakati.
Wasichana wananyimwa haki zao za
kupata elimu kutokana na tamaduni potofu'',alisema.
Aliongezea kuwa ukosefu wa hamasa
kuhusu maswala ya elimu miongoni mwa wazazi ni sababu nyengine ya wasichana
wengi wa shule kuwacha masomo katika jimbo hilo.
Amesema kwa kuwa wazazi
hawawahamasishi watoto wao kuhusu kwenda shule,wasichana wengi huwacha masomo
na kuolewa kupitia baraka za wazazi wao.
Afisa wa mradi wa TMEP Bi Valerie
Kalyalya amesema kuwa afisi yake itaendelea kutoa elimu kuhusu ngono kwa
wavulana na wasichana walio na umri wa zaidi ya miaka kumi.
No comments:
Post a Comment