Maandamano dhidi ya hatua ya kuahilisha uchaguzi |
Uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 28 mwezi Machi.
Mkuu
wa tume hiyo Attahiru Jega alisema kuwa amejulishwa na maafisa wa usalama kuwa
wanajeshi hawatakuwepo kulinda vituo vya kupigia kura kwa kuwa watakuwa
wakipigana na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi.
Awali
tume hiyo ilikuwa imetangaza kuwa haingewezekana kufunguliwa kwa vituo vya
kupigia kura katika maeneo ambapo maelfu ya watu tayari walikuwa wamehama.
Mwandishi
wa BBC anasema kuwa kuahrishwa kwa uchaguzi kutaleta utata kwa kuwa chama kikuu
cha upinzani kimekashifu jeshi kwa kulazimisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo ili
kumsaidia rais Goodluck Jonathan kufanya kampeni.
No comments:
Post a Comment