Bendera za nchi wanachama

Bendera za nchi wanachama

Thursday, April 30, 2015

KILIMO CHA MBOGAMBOGA


KILIMO CHA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Bi. Mariam Mohamed na Anita Mbigambo wakulima wa mbogamboga.
Wanawake 20 wa shirika la Tawodeo wamezalisha jumla ya tani 20 za mbogamboga licha ya kukabiliwa na changamoto ya wadudu waharibifu wa mboga mboga katika msimu wa kilimo mwaka 2014/2015.
Akizungumza na wanawake hao Mkurugenzi Mtendaji wa shilika hilo Bi.Anna Matenga amesema bado juhudi kubwa zinahitajika ili kuweza kuwaelimisha wanawake namna bora ya kilimo cha mbogamboga ikiwemo matumiza ya madawa ili kuweza kuwasaidia kuondokana na wadudu waharibifu.
Bi.Matenga amesema kilimo pekee kinaweza kuwa mkombozi kwa familia moja moja hasa wanawake kwani wengi wao ndio waangalizi wa familia katika kaya Vijijini.

Pakistan:Wanamgambo kifungoni

             Pakistan:Wanamgambo kifungoni

Malala Yousafzai alipigwa risasi ya kichwa na Wanamgambo wa Taliban
Mahakama moja ya Pakistan imewahukumu kifungo cha maisha wanamgambo 10 waliopatikana na hatia ya kuhusika katika tukio la miaka 3 iliyopita ,la kumshambulia kwa kumpiga risasi mwanaharakati wa kutetea haki za watoto, msichana Malala Yousafzai.
Wakati wa shambulio hilo ambapo alijeruhiwa vibaya sana baada ya kupigwa risasi ya kichwa , alikuwa na umri wa miaka 15 pekee .
Alilengwa na wanamgambo wa Taliban wa huko Pakistani kwa kuonekana kuwa mstari wa mbele kupigia kampeni ya kuendeleza elimu kwa wasichana.
Mwaka jana msichana Malala Yousafzai alitunukiwa tuzo la kimataifa la Nobel akiwa mshindi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hilo la amani Nobel Peace Prize.

Sunday, February 8, 2015

Uchaguzi mkuu waahirishwa Nigeria


Maandamano dhidi ya hatua ya kuahilisha uchaguzi
Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeahirisha uchaguzi mkuu ambao ulikuwa ufanyike tarehe 14 mwezi huu kutokana na sababu za kiusalama.
Uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 28 mwezi Machi.
Mkuu wa tume hiyo Attahiru Jega alisema kuwa amejulishwa na maafisa wa usalama kuwa wanajeshi hawatakuwepo kulinda vituo vya kupigia kura kwa kuwa watakuwa wakipigana na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi.
Awali tume hiyo ilikuwa imetangaza kuwa haingewezekana kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura katika maeneo ambapo maelfu ya watu tayari walikuwa wamehama.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kuahrishwa kwa uchaguzi kutaleta utata kwa kuwa chama kikuu cha upinzani kimekashifu jeshi kwa kulazimisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo ili kumsaidia rais Goodluck Jonathan kufanya kampeni.


Sunday, December 28, 2014

Mashindano ya Miss Tanzania yafungwa

Mashindano ya urembo nchini
Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Ndege ya Air Asia
Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta


Sunday, December 21, 2014

Mimba zawatoa wanafunzi shuleni Tanzania




Mschana Hakika Abdalah.

Takriban wasichana 808 wamewacha shule katika kipindi cha miaka minane katika jimbo la Rukwa nchini Tanzania kutokana na mimba ,mkuu wa elimu katika jimbo hilo Fanuel Mkaruka amesema.
Bwana Mkaruka amefichua hili wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu katika mkutano uliolenga kuzungumzia maswala muhimu ya elimu katika jimbo hilo.
Miongoni mwa maswala mengine, wadau walizungumzia changamoto zinazowakumba wanaume katika elimu ya ngono chini ya mradi wa TMEP.
Kulingana na Bwana Mkaruka ,idadi hiyo inashirikisha wasichana walioshika mimba na kuwacha shule katika ya mwaka 2010 na 2014.
Amesema kuwa idadi hiyo inashirikisha wasichana 59 kutoka shule za msingi na 749 kutoka shule za upili.
Nyumbani kwao Hakika Abdalah.
Ameongezea kuwa wilaya ya Nkasi ambayo ipo katika sehemu ya ziwa Tanganyika inaongoza na wasichana 477 ambao walishika mimba na kuwacha shule.
Aliongezea kwamba miongoni mwa wasichana 477,31 walikuwa wakisoma katika shule za msingi huku 446 wakiwa katika shule za upili.
Kulingana na Mkaruka ,tatizo hilo limekuwa likiongezeka kutokana utamaduni uliopitwa na wakati ambao unawaruhusu wazazi kuwaoza wanao hata iwapo wapo shuleni.
''Ni wazi kwamba tunakabiliwa na changamoto katika eneo hili,wazazi wengi bado wanaamini tamaduni ambazo tayari zimepitwa na wakati.
Wasichana wananyimwa haki zao za kupata elimu kutokana na tamaduni potofu'',alisema.
Aliongezea kuwa ukosefu wa hamasa kuhusu maswala ya elimu miongoni mwa wazazi ni sababu nyengine ya wasichana wengi wa shule kuwacha masomo katika jimbo hilo.
Amesema kwa kuwa wazazi hawawahamasishi watoto wao kuhusu kwenda shule,wasichana wengi huwacha masomo na kuolewa kupitia baraka za wazazi wao.
Afisa wa mradi wa TMEP Bi Valerie Kalyalya amesema kuwa afisi yake itaendelea kutoa elimu kuhusu ngono kwa wavulana na wasichana walio na umri wa zaidi ya miaka kumi.


Wasichana 100 waepuka tohara Tanzania


                                             
Umasikini na Ukeketeji watoto wa Kike

Zaidi ya wasichana mia moja wamehifadhiwa katika nyumba salama,baada ya kukimbia kuepuka tohara eneo la Kaskazini mwa Tanzania.Wasichana hao walilazimika kukwepa ibada hizo na hivyo kuondoka majumbani kwao kwa kuwa msimu umewadia na zoezi lazima litekelezwe.
Kwa muujibu wa desturi za serikali za mitaa,sheria ya kutahiri wanawake,ina maanisha ni kipindi cha mpito kwa binti kutoka kuwa msichana hadi mwanamke kamili,na hii inaashiria kwamba yuko tayari kwa kuolewa.
Wasicha mia moja kumi na nane kati yao wana umri wa miaka 10 hadi kumi na sita, wamehifadhiwa katika makazi salama na vituo vinavyoendeshwa na kanisa la Anglikan huko Mugumu, wilayani Serengeti.Rhobi Samwel ni mratibu wa mradi uitwao tunaweza ambao husghulika zaidi na kuupinga ukatili wa kijinsia.kwa muujibu Rhobi anaeleza kwamba mapema mwezi huu aliwaona mabinti hao wakiwa wamejikusanya kwenye vikundi,wengi wao wakiwa katika hali mbaya na hivyo kuwapeleka katika mazi salama.
Wasicha walio wengi wametokea wilayani Butiama,Tarime na Serengeti.miezi ya December na Januari ndio msimu wa tohara kwa wasichana na wavulana kwa mkoa wa Mara.viongozi wa maeneo husika wansema kwamba kupambana na kitu kinachoonekana kama ibada ya kitamaduni utamaduni ni suala nyeti na endelevu .
Sijali Nyambuche ni afisa wa polisi anayeshughulikia dawati la masuala ya jinsia na uangalizi wa wanawake na watoto huko Mugumu,Serengeti.Yeye anasema pamoja na masuala yanayohusiana na hatari za kiafya,jamii zimeendelea kushikilia msimamo wa kudumisha mila hiyo isiyo faa na hivyo kudumaza juhudi za kumaliza tohara mkoani humo.Sophia Simba, waziri wa maendeleo ya jinisa na watoto ana fafanua juu ya ukweli kuwa mara nyingi wasichana hukutwa wakiwa tayari wameshafanyiwa tohara ;
Kwa muujibu wa sheria ya makosa maalumu sheria ya mwaka 1998 ina kinza suala la tohara hutekelezwa kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18,lakini sheria hiyo haitoi ulinzi ama tamko lolote mara baada ya wasichana hao wanapovuka kizingiti cha umri huo.adhabu kwa kosa la tohara ni kifungo cha miaka mitano hadi kumi na mitano .Ukatili huu umekuwa ukipungua tangu nchi ya Tanzania ilipopiga marufuku vitendo hivyo mnamo mwaka 1996 na hii imechangiwa na kampeni za kuijengea uwezo na kuielimisha jamii zilizokuwa zikiendeshwa na vikundi vya haki za binaadamu .