Bendera za nchi wanachama

Bendera za nchi wanachama

Sunday, December 28, 2014

Mashindano ya Miss Tanzania yafungwa

Mashindano ya urembo nchini
Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Ndege ya Air Asia
Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta


Sunday, December 21, 2014

Mimba zawatoa wanafunzi shuleni Tanzania




Mschana Hakika Abdalah.

Takriban wasichana 808 wamewacha shule katika kipindi cha miaka minane katika jimbo la Rukwa nchini Tanzania kutokana na mimba ,mkuu wa elimu katika jimbo hilo Fanuel Mkaruka amesema.
Bwana Mkaruka amefichua hili wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu katika mkutano uliolenga kuzungumzia maswala muhimu ya elimu katika jimbo hilo.
Miongoni mwa maswala mengine, wadau walizungumzia changamoto zinazowakumba wanaume katika elimu ya ngono chini ya mradi wa TMEP.
Kulingana na Bwana Mkaruka ,idadi hiyo inashirikisha wasichana walioshika mimba na kuwacha shule katika ya mwaka 2010 na 2014.
Amesema kuwa idadi hiyo inashirikisha wasichana 59 kutoka shule za msingi na 749 kutoka shule za upili.
Nyumbani kwao Hakika Abdalah.
Ameongezea kuwa wilaya ya Nkasi ambayo ipo katika sehemu ya ziwa Tanganyika inaongoza na wasichana 477 ambao walishika mimba na kuwacha shule.
Aliongezea kwamba miongoni mwa wasichana 477,31 walikuwa wakisoma katika shule za msingi huku 446 wakiwa katika shule za upili.
Kulingana na Mkaruka ,tatizo hilo limekuwa likiongezeka kutokana utamaduni uliopitwa na wakati ambao unawaruhusu wazazi kuwaoza wanao hata iwapo wapo shuleni.
''Ni wazi kwamba tunakabiliwa na changamoto katika eneo hili,wazazi wengi bado wanaamini tamaduni ambazo tayari zimepitwa na wakati.
Wasichana wananyimwa haki zao za kupata elimu kutokana na tamaduni potofu'',alisema.
Aliongezea kuwa ukosefu wa hamasa kuhusu maswala ya elimu miongoni mwa wazazi ni sababu nyengine ya wasichana wengi wa shule kuwacha masomo katika jimbo hilo.
Amesema kwa kuwa wazazi hawawahamasishi watoto wao kuhusu kwenda shule,wasichana wengi huwacha masomo na kuolewa kupitia baraka za wazazi wao.
Afisa wa mradi wa TMEP Bi Valerie Kalyalya amesema kuwa afisi yake itaendelea kutoa elimu kuhusu ngono kwa wavulana na wasichana walio na umri wa zaidi ya miaka kumi.


Wasichana 100 waepuka tohara Tanzania


                                             
Umasikini na Ukeketeji watoto wa Kike

Zaidi ya wasichana mia moja wamehifadhiwa katika nyumba salama,baada ya kukimbia kuepuka tohara eneo la Kaskazini mwa Tanzania.Wasichana hao walilazimika kukwepa ibada hizo na hivyo kuondoka majumbani kwao kwa kuwa msimu umewadia na zoezi lazima litekelezwe.
Kwa muujibu wa desturi za serikali za mitaa,sheria ya kutahiri wanawake,ina maanisha ni kipindi cha mpito kwa binti kutoka kuwa msichana hadi mwanamke kamili,na hii inaashiria kwamba yuko tayari kwa kuolewa.
Wasicha mia moja kumi na nane kati yao wana umri wa miaka 10 hadi kumi na sita, wamehifadhiwa katika makazi salama na vituo vinavyoendeshwa na kanisa la Anglikan huko Mugumu, wilayani Serengeti.Rhobi Samwel ni mratibu wa mradi uitwao tunaweza ambao husghulika zaidi na kuupinga ukatili wa kijinsia.kwa muujibu Rhobi anaeleza kwamba mapema mwezi huu aliwaona mabinti hao wakiwa wamejikusanya kwenye vikundi,wengi wao wakiwa katika hali mbaya na hivyo kuwapeleka katika mazi salama.
Wasicha walio wengi wametokea wilayani Butiama,Tarime na Serengeti.miezi ya December na Januari ndio msimu wa tohara kwa wasichana na wavulana kwa mkoa wa Mara.viongozi wa maeneo husika wansema kwamba kupambana na kitu kinachoonekana kama ibada ya kitamaduni utamaduni ni suala nyeti na endelevu .
Sijali Nyambuche ni afisa wa polisi anayeshughulikia dawati la masuala ya jinsia na uangalizi wa wanawake na watoto huko Mugumu,Serengeti.Yeye anasema pamoja na masuala yanayohusiana na hatari za kiafya,jamii zimeendelea kushikilia msimamo wa kudumisha mila hiyo isiyo faa na hivyo kudumaza juhudi za kumaliza tohara mkoani humo.Sophia Simba, waziri wa maendeleo ya jinisa na watoto ana fafanua juu ya ukweli kuwa mara nyingi wasichana hukutwa wakiwa tayari wameshafanyiwa tohara ;
Kwa muujibu wa sheria ya makosa maalumu sheria ya mwaka 1998 ina kinza suala la tohara hutekelezwa kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18,lakini sheria hiyo haitoi ulinzi ama tamko lolote mara baada ya wasichana hao wanapovuka kizingiti cha umri huo.adhabu kwa kosa la tohara ni kifungo cha miaka mitano hadi kumi na mitano .Ukatili huu umekuwa ukipungua tangu nchi ya Tanzania ilipopiga marufuku vitendo hivyo mnamo mwaka 1996 na hii imechangiwa na kampeni za kuijengea uwezo na kuielimisha jamii zilizokuwa zikiendeshwa na vikundi vya haki za binaadamu .



Saturday, December 20, 2014

Rihanna aajiriwa na kampuni ya Puma

Riahana msanii wa Marekani aajiliwa na kampuni ya Puma

Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.
Ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.
Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao wenyewe.
Riahana Msaani wa Marekani

Jukumu la Rihana litakuwa kuwa na ushawishi katika bidhaa zitakazoundwa pamoja na kuandaa ukuzaji wa bidhaa mpya.
Akiwa miongoni mwa kampeni ya Forever faster msanii huyo atashirikishwa na wanariadha kama viule Usain Bolt na Sergio Aguero.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bjorn Gulden amesema kuwa waliamua kumtafuta mshirika katika nguo za wanawake za kufanyia mazoezi kutokana na ushawishi mkubwa wa kampuni hiyo katika soka,riadha na mashindano ya magari.
Tunafurahi kumpata Rihana na tunajianda kuona ni nini tunaweza buni kwa ushirikiano wake.
Rihana si mtu wa kwanza nje ya michezo kujiunga na kampuni ya Puma.
Msanii 50 cent na Jay Z walitoa viatu na kampuni ya Reebok, huku Kim Kardashian akiwa uso wa viatu vya Sketchers na mumewe Kanye West akifanya kazi na Nike pamoja na Adidas.


Friday, December 19, 2014

Kenyatta asaini sheria kali ya usalama

Rais Uhuru Kenyatta
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab. Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.                                                                                                          Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.                                                                                                                Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.                                                                                                               Vyombo vya habari vimesema baadhi ya vipengee vya sheria hio ninabana uhuru wa vyombo vya habari na hata kutishia kwenda mahakamani.Mswada huo kabla ya kutiwa saini na kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na katiba.                                                                                                                 Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.Polisi pia ndio watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au kuonyeshwa katika vyombo vya habari.                                                                                                                       Vyombo vya habaro vinasema haya yanakwenda kinyume na uhueu wa vyombo vya habari.Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu.

Sarakasi mpya ya Escrow


Rais wa Tanzania Kikwete


Wakati Taifa likisubiri kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa Serikali waliohusishwa na kashfa ya Akaunti ya Escrow, Kampuni za IPTL na Pan Africa Power Solutions (PAP) zimekimbilia mahakamani kuzuia utekelezaji wa maazimio hayo.
Kampuni hizo kwa kushirikiana na Harbinder Singh Seth zimefungua kesi ya kikatiba Katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga utekelezaji wa maazimio hayo.
Kesi hiyo imefunguliwa siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu wadhifa huo akisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.
Pia ni katika kipindi ambacho kuna taarifa zilizothibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuwa Rais Kikwete atazungumzia suala hilo wakati wowote kabla ya kesho.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao ya kijamii Rais Kikwete atazungumza kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo, lakini Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu alipoulizwa jana hakukanusha wala kukubali akisema ikitokea Rais anataka kuzungumza vyombo vya habari vitataarifiwa.
Tayari Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa ziarani Uarabuni amerejea nchini jana mchana baada ya ziara yake kukatishwa na Rais Kikwete kwa shughuli maalumu na anatarajiwa kurudi tena Falme za Kiarabu kesho kuendelea na ziara yake hadi Desemba 23, mwaka huu.
Kesi yenyewe
Katika kesi hiyo namba 59 ya mwaka 2014, iliyofunguliwa chini ya hati ya dharura jana, kampuni hizo zinawakilishwa na mawakili kutoka kampuni za uwakili za Bulwark Associates Advocates, Asyla Attorneys na Marando, Mnyele & Co. Advocates za Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, kampuni hizo zinadai kuwa kile kilichofanyika ndani ya Bunge, kujadili na kupitisha maazimio dhidi ya watuhumiwa hao, ni kinyume cha Katiba na kwamba kina lengo la kugombanisha mihimili mitatu ya dola.
Kampuni hiyo zinadai kuwa kulikuwa na kesi ambazo zinaendelea mahakamani zinazohusu suala ambalo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Takukuru walifanyia uchunguzi na hatimaye taarifa ya CAG kujadiliwa bungeni na kutolewa maazimio hayo.
Maazimio ya Bunge ni pamoja na kutaka waliohusika wawajibike kwa mujibu wa sheria, Serikali iangalie uwezekano wa kutaifisha na kuifanya mitambo ya IPTL imilikiwe na Serikali, ipitie upya mikataba yote na kuangalia kama ina masilahi na Taifa na iboreshwe.
IPTL na PAP zimesema kitendo hicho cha kujadili na kutoa maazimio kilipuuza amri ya Mahakama Kuu kwa kufuata tafsiri potofu iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha - Rose Migiro kuhusu amri ya Mahakama hiyo, ambayo ilizua mjadala wa escrow kujadiliwa bungeni.

Wednesday, December 17, 2014

Wakulima wa karafuu,Pemba waomba msaada

Wakulima wa karafuu,Pemba waomba msaada
Zao la karafuu kisiwani Pemba.


Kisiwa kidogo kilichoko Bahari ya Hindi, Pemba kimekuwa mzalishaji mkubwa wa karafuu duniani kwa miaka mingi. Hivi karibuni umaarufu huo umepigwa kumbo na Indonesia. Wakulima Pemba wanasema wanaitaka Serikali yao kufanya juhudi kwa ajili ya kuendeleza zao ambalo wamekuwa wakizalisha kwa miaka mingi. Mengi zaidi ni katika taarifa yake Salim Kikeke kutoka Pemba.
Rais wa Zanzibara Dr. Ali Muhamed Shein akipima karafuu

Tuesday, December 16, 2014

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana, Jumanne, kufuatia sakata la uchotaji wa fedha kutoka akaunti ya ESCROW ambapo zaidi ya dola milioni 120 zilihamishwa.
Mwanasheria mkuu, pamoja na baadhi ya wanasiasa na maafisa waandamizi wa serikali walituhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha kufanyika kwa miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta.
Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frediriki Welema
Leonard Mubali ameandaa taarifa ifuatayo:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali.
Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Jaji Werema amesema ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali ilipeleka pendekezo kumtaka Jaji Werema kuwajibika
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Kamati ya Bunge ya hesabu za serikali ilipeleka mapendekezo ya kumtaka Jaji Welema awajibike
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe
Kamati hiyo ya Bunge pia ilipendekeza kuwa waziri wa Nishati na Madini, waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwanasheria mkuu, katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya hesabu za serikali Zitto Kabwe
Pia maazimio ya Kamati ya kudumu ya bunge ilipendekeza kuwa, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na makampuni binafsi imeisababishia Tanesco hasara ya mabilioni ya fedha na kutishia uhai wake wa kifedha, serikali iwasilishe mikataba husika bungeni au kwenye kamati zake kwa lengo la kutekeleza vema wajibu wake wa kuimamia na kuishauri serikali.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.

Saturday, December 13, 2014

Watoto wakike wahimizwa kusoma kwa bidii.


Sekta ya Uvuvi inavyo wasaidia wanawake Mkoa wa Kigoma.

Wavuvi ziwa Tanganyika 

                                
                                                  Dagaa wameanikwa                                                              
 Wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Kigoma wanaonufaika kupitia rasilimali Samaki na Dagaa kutoka ziwa Tanganyika wakiwa katika Biashara yao ya kila siku.
Mpaka sasa wastani wa wanawake 20 wanategemea mapato yatokanayo na biashara ya dagaa na Samaki. wanawake hao wamefakinikiwa kupata makazi ya kudumu pamoja na fedha za kulipia karo za shule katika familia zao.

Maendeleo ya Wanawake hayaji kwa kukaa majumbani tu.


Utalii wa endelea kuwa kivutio kikubwa Tanzania






Watoto ni kiyoo cha maendeleo ya kizazi cha kesho.