Wasichana wapewe kipaumbele katika sekta ya elimu |
Bendera za nchi wanachama
Wednesday, October 14, 2015
Elimu kwa wasichana iboreshwe Tanzania
Wanawake waandamana Uganda
Wanawake waandamana nchini Uganda |
Kundi la wanawake nchini Uganda wanaopinga kuvuliwa nguo kwa mwenzao wakati alipokuwa akikamatwa na maafisa wa polisi, limefanya maandamano na kujaribu kuelekea bungeni ili kuwasilisha hoja yao dhidi ya ukatili wa maafisa wa polisi.
Hatua hiyo inajiri baada ya mwanamke mmoja kutoka chama cha Upinzani cha Forum for Democratic Change kinachoongozwa na Kizza Besigye kuvuliwa nguo na maafisa wa polisi alipokuwa akikamatwa wikendi iliopita.
Waandamana Uganda |
Hatahivyo waandamanaji hao walizuiliwa kuendeleza maandamano hayo na kusukumwa hadi katika afisi zao na maafisa wa polisi.
Kulikuwa na jaribio la kuwakamata baadhi yao lakini walikataa.
Thursday, August 20, 2015
Kufanya kazi kwa saa nyingi ni hatari
Wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wako hatarini kupata kiharusi |
Utafiti umeeleza kuwa Watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi,utafiti huo ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano.
takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu,Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.
Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.
Dokta Mika Kivimaki , kutoka Chuo cha jijni London.
Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.
Daktari Kivimaki ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa watu wanapaswa kuwa makini na afya zao,kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.
takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu,Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.
Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.
Dokta Mika Kivimaki , kutoka Chuo cha jijni London.
Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.
Daktari Kivimaki ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa watu wanapaswa kuwa makini na afya zao,kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.
Monday, August 17, 2015
Nancy mshindi Tuzo la Komla Dumor
Mshindi wa Tuzo la BBC World News Komla Dumor Award |
Mwanahabari kutoka Uganda, Nancy Kacungira ni mshindi wa Tuzo la kwanza la kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Komla Dumor.
Tuzo hilo BBC World News Komla Dumor Award, lina lengo la kuendelea kuimarisha uandishi wa habari kuhusu Afrika.
Mtangazaji huyu wa kituo cha televisheni cha KTN cha Kenya,alichaguliwa miongoni mwa washiriki wapatao 200.
Nancy Kacungira ni mtangazaji habari wa kituo cha televisheni cha KTN |
Mshindi huyo atakuwa makao makuu ya BBC, mjini London kwa miezi mitatu na pia kutuma taarifa za habari za BBC Televisheni , radio na mtandao kutoka barani Afrika.
Tuzo hilo lilianzishwa ili kumuenzi Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41.
Bi Kacungira alisema: " nimeshtushwa, lakini pia kufurahishwa sana kwa kupokea habari hizi.
Nimepokea kwa unyenyekevu mkubwa ushindi wa tuzo hili".
"Hili ni tuzo la bara hili ninalolipenda na ambalo nimejitolea kulihudumia, kwa kutekeleza jukumu langu la kutoa taswira halisi ya bara ambalo kwa muda mrefu taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa na kuongezewa chumvi.'
"Kuwa sehemu ya kumbukumbu ya Komla ni heshima kubwa, nikama ndoto.''
''Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili kuthibitisha uaminifu niliyoonyeshwa kwa kupewa tuzo hilo.''
'Pia nitahakikisha kwamba mazao yake hayanifaidi mimi tu".
Wahariri wamsifu
Mmoja ya waamuzi, Mhariri wa habari, wa Idhaa ya BBC Afrika, Vera Kwakofi,alimsifu bi Kacungira.
'' Nancy ni mwerevu sana na ana upeo mpana wa mawazo na ujuzi unaojitokeza mara moja."
"Nimefurahi kwamba katika Nancy tumempata mwanahabari mwenye kipaji na ari,
''mtu anayestahili kuwa mshindi wa tuzo tulilolianzisha kwa jina la Komla."
Nancy amekulia Uganda ambapo alihitimu kutoka chuo kikuu cha Makerere, mjini Kampala.
Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41 |
Ana ujuzi wa zaidi ya miaka 14 katika fani ya uwanahabari kwani amefanya kazi katika mshirika kadha ya habari nchini Kenya, Uganda na Tanzania.
Pia ana shahada ya uzamifu katika mawasiliano kutoka chuo kikuu cha Leeds.
Kwa wakati huu yeye ni mtangazaji wa habari za usiku za Kiingereza katika kituo cha televisheni cha KTN na pia ni mhariri wa mtandao wa Kijamii wa shirika hilo.
Washiriki wawili waliibuka nambari mbili: Leila Dee Dougan kutoka Afrika Kusini na Paa Kwesi Asare kutoka Ghana.
Komla hasahauliki
Komla Dumor alikuwa mtangazaji raia wa Ghana mwenye kipaji cha kipekee ambaye katika maisha yake mafupi alikuwa na mvuto wa ajabu nchini Ghana, Afrika na ulimwenguni.
Aliwakilisha ule upande wa Afrika wa ujasiriamali na umahiri.
Kutokana na uwanahabari wake dhabiti na kipaji chake cha kuelezea habari kwa uweledi mkubwa , Komla alifanya kazi bila kuchoka ili kutoa taswira halisi ya Afrika kwa ulimwengu.
BBC inashukuru shirika la Standard Chartered na wahisani wengine kwa misaada yao.
Monday, May 25, 2015
MWANA DADA WEMA SEPETU APATA TUZO 2015
Friday, May 22, 2015
Changia ujenzi wa kituo cha kulele watoto yatima Kibondo
WANAWAKE KATIKA HABARI PICHA
Je! Wanawake hawa wataweza kujikwamua kiuchumi ? |
Je! Bado huna matumaini dhidi ya mfano huu bora wa wanawake? |
Jibu la kweli ndio kilimo kimeweza kukwamua Uchumi wa wanawake kibiashara hivyo kila mmoja anaweza kukucha kipato chake kwa kuanzisha bustani za mbogamboga (Picha na Meneja mradi Bi. Anna Matenga) |
Thursday, April 30, 2015
KILIMO CHA MBOGAMBOGA
KILIMO CHA KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Bi. Mariam Mohamed na Anita Mbigambo wakulima wa mbogamboga. |
Akizungumza na wanawake hao Mkurugenzi Mtendaji wa shilika hilo Bi.Anna Matenga amesema bado juhudi kubwa zinahitajika ili kuweza kuwaelimisha wanawake namna bora ya kilimo cha mbogamboga ikiwemo matumiza ya madawa ili kuweza kuwasaidia kuondokana na wadudu waharibifu.
Bi.Matenga amesema kilimo pekee kinaweza kuwa mkombozi kwa familia moja moja hasa wanawake kwani wengi wao ndio waangalizi wa familia katika kaya Vijijini.
Pakistan:Wanamgambo kifungoni
Pakistan:Wanamgambo
kifungoni
Malala Yousafzai alipigwa risasi ya kichwa na Wanamgambo wa Taliban |
Mahakama
moja ya Pakistan imewahukumu kifungo cha maisha wanamgambo 10 waliopatikana na
hatia ya kuhusika katika tukio la miaka 3 iliyopita ,la kumshambulia kwa
kumpiga risasi mwanaharakati wa kutetea haki za watoto, msichana Malala
Yousafzai.
Wakati
wa shambulio hilo ambapo alijeruhiwa vibaya sana baada ya kupigwa risasi ya
kichwa , alikuwa na umri wa miaka 15 pekee .
Alilengwa
na wanamgambo wa Taliban wa huko Pakistani kwa kuonekana kuwa mstari wa mbele
kupigia kampeni ya kuendeleza elimu kwa wasichana.
Mwaka
jana msichana Malala Yousafzai alitunukiwa tuzo la kimataifa la Nobel akiwa
mshindi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hilo la amani Nobel Peace
Prize.
Sunday, February 8, 2015
Uchaguzi mkuu waahirishwa Nigeria
Maandamano dhidi ya hatua ya kuahilisha uchaguzi |
Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeahirisha uchaguzi mkuu ambao ulikuwa ufanyike tarehe 14 mwezi huu kutokana na sababu za kiusalama.
Uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 28 mwezi Machi.
Mkuu
wa tume hiyo Attahiru Jega alisema kuwa amejulishwa na maafisa wa usalama kuwa
wanajeshi hawatakuwepo kulinda vituo vya kupigia kura kwa kuwa watakuwa
wakipigana na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi.
Awali
tume hiyo ilikuwa imetangaza kuwa haingewezekana kufunguliwa kwa vituo vya
kupigia kura katika maeneo ambapo maelfu ya watu tayari walikuwa wamehama.
Mwandishi
wa BBC anasema kuwa kuahrishwa kwa uchaguzi kutaleta utata kwa kuwa chama kikuu
cha upinzani kimekashifu jeshi kwa kulazimisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo ili
kumsaidia rais Goodluck Jonathan kufanya kampeni.
Subscribe to:
Posts (Atom)