Bendera za nchi wanachama

Bendera za nchi wanachama

Monday, May 25, 2015

MWANA DADA WEMA SEPETU APATA TUZO 2015


WEMA SEPETU NA ELIZABETH MAICO (LULU) WAMG'ARA NA TUNZO 2015

Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa ameshika tuzo yake.
MKURUGENZI wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina yake baada ya kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper, Elizabeht Michael ‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu.

Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa na Meneja wake Martin Kadinda. Akizungumza kwa furaha muda mfupi baada ya kutwaa tuzo hiyo, Wema alisema kwamba amefurahia kuwa mshindi na amejisikia vizuri kwani hakutarajia kuibuka kidedea, ila anaamini mashabiki wake ndiyo waliomfanya akashinda na kuahidi kuwa nao bega kwa bega.

“Nashukuru sana kwa kutwaa tuzo hii ambayo kwa namna moja au nyingine naiona kama sapraizi maana tulikuwa tukigombea wengi, ila mashabiki wangu wameniwezesha kwa kiasi kikubwa kuitwaa tuzo hii, ninachoweza kusema kwa sasa nashukuru sana uongozi wa Endless Fame hususan meneja na wafanyakazi wangu wote,” alisema Wema.





Friday, May 22, 2015

Changia ujenzi wa kituo cha kulele watoto yatima Kibondo

Watoto 30 yatima na wale waishio katika Mazingira magumu Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wanahitaji makazii maalumu yaliyo na huduma bora za kibinadamu kufuatia kukosa wazazi na wengine kukosa usaidizi wa familia zao baada ya kutelekezwa na wazazi wao, Hivyo ungana na Shirika la Maendeleo ya Wanawake Tanzania (TAWODEO)............... "Kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima"
Usimamizi wa watoto unafanywa na Jamii ili kuweza kuleta mabadiliko ya kizazi kwa matumaini ya kuwepo kwa jamii iliyo bora hapo baadae.(Picha na Meneja Mradi Bi. Anna Matenga)

WANAWAKE KATIKA HABARI PICHA

Je! Wanawake hawa wataweza kujikwamua kiuchumi ?
Je! Bado huna matumaini dhidi ya mfano huu bora wa wanawake?
Jibu la kweli ndio kilimo kimeweza kukwamua Uchumi wa wanawake kibiashara hivyo kila mmoja anaweza kukucha kipato chake kwa kuanzisha bustani za mbogamboga (Picha na Meneja mradi Bi. Anna Matenga)