Bendera za nchi wanachama

Bendera za nchi wanachama

Wednesday, October 14, 2015

Elimu kwa wasichana iboreshwe Tanzania

Wasichana wapewe kipaumbele katika sekta ya elimu
Idadi ya wanafunzi wakike wanao maliza elimu ya sekondari imeongezeka Wilayani kibondo licha ya wasichana wengi kupata ufauru mzuri kwaajili kuendelea masomo ngazi ya juu.

Wanawake waandamana Uganda

Wanawake waandamana nchini Uganda
Kundi la wanawake nchini Uganda wanaopinga kuvuliwa nguo kwa mwenzao wakati alipokuwa akikamatwa na maafisa wa polisi, limefanya maandamano na kujaribu kuelekea bungeni ili kuwasilisha hoja yao dhidi ya ukatili wa maafisa wa polisi.
Hatua hiyo inajiri baada ya mwanamke mmoja kutoka chama cha Upinzani cha Forum for Democratic Change kinachoongozwa na Kizza Besigye kuvuliwa nguo na maafisa wa polisi alipokuwa akikamatwa wikendi iliopita.
Waandamana Uganda
Hatahivyo waandamanaji hao walizuiliwa kuendeleza maandamano hayo na kusukumwa hadi katika afisi zao na maafisa wa polisi.
Kulikuwa na jaribio la kuwakamata baadhi yao lakini walikataa.

Thursday, August 20, 2015

Kufanya kazi kwa saa nyingi ni hatari

Wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wako hatarini kupata kiharusi
Utafiti umeeleza kuwa Watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi,utafiti huo ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano.
takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu,Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.
Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.
Dokta Mika Kivimaki , kutoka Chuo cha jijni London.
Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.
Daktari Kivimaki ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa watu wanapaswa kuwa makini na afya zao,kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.

Monday, August 17, 2015

Nancy mshindi Tuzo la Komla Dumor

Mshindi wa Tuzo la BBC World News Komla Dumor Award
Mwanahabari kutoka Uganda, Nancy Kacungira ni mshindi wa Tuzo la kwanza la kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Komla Dumor.
Tuzo hilo BBC World News Komla Dumor Award, lina lengo la kuendelea kuimarisha uandishi wa habari kuhusu Afrika.
Mtangazaji huyu wa kituo cha televisheni cha KTN cha Kenya,alichaguliwa miongoni mwa washiriki wapatao 200.
Nancy Kacungira ni mtangazaji habari wa kituo cha televisheni cha KTN
Mshindi huyo atakuwa makao makuu ya BBC, mjini London kwa miezi mitatu na pia kutuma taarifa za habari za BBC Televisheni , radio na mtandao kutoka barani Afrika.
Tuzo hilo lilianzishwa ili kumuenzi Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41.
Bi Kacungira alisema: " nimeshtushwa, lakini pia kufurahishwa sana kwa kupokea habari hizi.
Nimepokea kwa unyenyekevu mkubwa ushindi wa tuzo hili".
"Hili ni tuzo la bara hili ninalolipenda na ambalo nimejitolea kulihudumia, kwa kutekeleza jukumu langu la kutoa taswira halisi ya bara ambalo kwa muda mrefu taarifa zake zimekuwa zikipotoshwa na kuongezewa chumvi.'
"Kuwa sehemu ya kumbukumbu ya Komla ni heshima kubwa, nikama ndoto.''
''Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili kuthibitisha uaminifu niliyoonyeshwa kwa kupewa tuzo hilo.''
'Pia nitahakikisha kwamba mazao yake hayanifaidi mimi tu".

Wahariri wamsifu

Mmoja ya waamuzi, Mhariri wa habari, wa Idhaa ya BBC Afrika, Vera Kwakofi,alimsifu bi Kacungira.
'' Nancy ni mwerevu sana na ana upeo mpana wa mawazo na ujuzi unaojitokeza mara moja."
"Nimefurahi kwamba katika Nancy tumempata mwanahabari mwenye kipaji na ari,
''mtu anayestahili kuwa mshindi wa tuzo tulilolianzisha kwa jina la Komla."
Nancy amekulia Uganda ambapo alihitimu kutoka chuo kikuu cha Makerere, mjini Kampala.
Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41
Ana ujuzi wa zaidi ya miaka 14 katika fani ya uwanahabari kwani amefanya kazi katika mshirika kadha ya habari nchini Kenya, Uganda na Tanzania.
Pia ana shahada ya uzamifu katika mawasiliano kutoka chuo kikuu cha Leeds.
Kwa wakati huu yeye ni mtangazaji wa habari za usiku za Kiingereza katika kituo cha televisheni cha KTN na pia ni mhariri wa mtandao wa Kijamii wa shirika hilo.
Washiriki wawili waliibuka nambari mbili: Leila Dee Dougan kutoka Afrika Kusini na Paa Kwesi Asare kutoka Ghana.

Komla hasahauliki
Komla Dumor alikuwa mtangazaji raia wa Ghana mwenye kipaji cha kipekee ambaye katika maisha yake mafupi alikuwa na mvuto wa ajabu nchini Ghana, Afrika na ulimwenguni.
Aliwakilisha ule upande wa Afrika wa ujasiriamali na umahiri.
Kutokana na uwanahabari wake dhabiti na kipaji chake cha kuelezea habari kwa uweledi mkubwa , Komla alifanya kazi bila kuchoka ili kutoa taswira halisi ya Afrika kwa ulimwengu.
BBC inashukuru shirika la Standard Chartered na wahisani wengine kwa misaada yao.

Monday, May 25, 2015

MWANA DADA WEMA SEPETU APATA TUZO 2015


WEMA SEPETU NA ELIZABETH MAICO (LULU) WAMG'ARA NA TUNZO 2015

Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa ameshika tuzo yake.
MKURUGENZI wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina yake baada ya kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper, Elizabeht Michael ‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Watu.

Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa na Meneja wake Martin Kadinda. Akizungumza kwa furaha muda mfupi baada ya kutwaa tuzo hiyo, Wema alisema kwamba amefurahia kuwa mshindi na amejisikia vizuri kwani hakutarajia kuibuka kidedea, ila anaamini mashabiki wake ndiyo waliomfanya akashinda na kuahidi kuwa nao bega kwa bega.

“Nashukuru sana kwa kutwaa tuzo hii ambayo kwa namna moja au nyingine naiona kama sapraizi maana tulikuwa tukigombea wengi, ila mashabiki wangu wameniwezesha kwa kiasi kikubwa kuitwaa tuzo hii, ninachoweza kusema kwa sasa nashukuru sana uongozi wa Endless Fame hususan meneja na wafanyakazi wangu wote,” alisema Wema.





Friday, May 22, 2015

Changia ujenzi wa kituo cha kulele watoto yatima Kibondo

Watoto 30 yatima na wale waishio katika Mazingira magumu Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wanahitaji makazii maalumu yaliyo na huduma bora za kibinadamu kufuatia kukosa wazazi na wengine kukosa usaidizi wa familia zao baada ya kutelekezwa na wazazi wao, Hivyo ungana na Shirika la Maendeleo ya Wanawake Tanzania (TAWODEO)............... "Kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima"
Usimamizi wa watoto unafanywa na Jamii ili kuweza kuleta mabadiliko ya kizazi kwa matumaini ya kuwepo kwa jamii iliyo bora hapo baadae.(Picha na Meneja Mradi Bi. Anna Matenga)

WANAWAKE KATIKA HABARI PICHA

Je! Wanawake hawa wataweza kujikwamua kiuchumi ?
Je! Bado huna matumaini dhidi ya mfano huu bora wa wanawake?
Jibu la kweli ndio kilimo kimeweza kukwamua Uchumi wa wanawake kibiashara hivyo kila mmoja anaweza kukucha kipato chake kwa kuanzisha bustani za mbogamboga (Picha na Meneja mradi Bi. Anna Matenga)